Image
Image

Rais Erdogan atoa wito wa amani kwa viongozi wa kimataifa waliohudhuria kongamano la nishati

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alitoa hotuba kwenye kongamano la 23 la dunia la nishati lililofanyika mjini Istanbul.Erdogan alizungumzia suala la mapambano dhidi ya ugaidi na kuhimiza jumuiya ya kimataifa kuweka ushirikiano ili kusaidia kutatua tatizo hilo la ulimwengu.
Akisisitiza umuhimu wa kuweka ushirikiano, Erdogan alisema, ‘‘Tushikamane pamoja ili kutatua mzozo wa Syria na Iraq na kudumisha amani.’’
Katika hotuba yake, Erdogan aliongezea kusema, ‘‘Kama tunavyojumuika pamoja kwa ajili ya kukuza sekta ya nishati, vivyo hivyo tunapaswa kuungana kwa ajili ya mapambano dhidi ya ugaidi.’’
Rais Erdogan pia alibainisha matumaini ya Uturuki ya kuimarisha uwekezaji katika sekta ya nishati.
Erdogan alisema, ‘‘Uturuki ina uwezo mkubwa katika suala la uwekezaji. Hivyo basi, yeyote atakayewekeza Uturuki hawezi kujutia kamwe.’’
Erdogan pia aliarifu mpango wa kutekeleza mradi wa ujenzi wa kituo cha 3 cha nyuklia na kukidhi asilimia 10 ya mahitaji ya nishati ya Uturuki.
Akibainisha kuendelezwa kwa mchakato wa usafirishaji gesi  kupitia Uturuki, Erdogan alisema, ‘‘Tumeweza kufanikisha mradi wa Azeri Petrol kwa ajili ya mabomba ya usafirishaji kati ya Baku-Tbilisi-Ceyhan. Kwa sasa ujenzi wa TANAP unaendelea ambapo gesi ya Azeri itaweza kusafirishwa Ulaya kupitia Uturuki.’’
Wakati huo huo, rais Erdogan akishirikiana pamoja na rais Vladimir Putin wa Urusi, rais Nicolas Maduro wa Venezuela, rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan na rais Mustafa Akıncı wa Cyprus, walitoa ujumbe wa amani kwaulimwengu mzima.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment