Tarehe 11 Octoba
ya kila mwaka inakuwa ni siku ya maadhimisho ya mtoto wa Kike duniani
kote huku yakilenga kuelimisha na kuhamasisha jamii kutambua haki za
mtoto wa kike ambapo Kitaifa maadhimisho haya yanafanyika mkoani
Shinyanga.
Katika Kuelekea kilele cha siku ya mtoto wa kike duniani
Mkoani Shinyanga Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii,
Jinsia,Wazee na Watoto, SIHABA NKINGA amekutana na baadhi ya
wadau wa afya ya uzazi Wilayani Kahama kuweka mikakati ya kuzuia na
kupambana na mimba na ndoa za utotoni.
Wadau wa afya ya uzazi Mkoani
Shinyanga wamesema lengo kuu la kufanya miradi ya afya katika jamii ni
kukumbushana madhara yanayosababishwa na mimba na ndoa za utotoni huku
baadhi ya wanafunzi wakiwataka wazazi kuwawekea miundombinu bora ya
elimu pamoja na kuwatimizia mahitaji yao.
Kauli mbiu katika siku ya mtoto wa kike ni “mimba na ndoa za utotoni zinaepukika,chukua hatua kumlinda mtoto wa kike.
Home
News
Slider
Dunia leo inaadhimisha Siku ya mtoto wa kike ambapo kwa Tanzania kitaifa inaadhimishwa Shinyanga.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment