Image
Image

Ufaransa yashutumiwa na mashirika ya kutetea haki za kibinadamu kwa kukataa kupokea wahamiaji

Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu yameishutumu Ufaransa kwa kukataa kufungua milango na kuwapokea wahamiaji waliofurika mpakani mwa Italia.Mashirika hayo yanayojumuisha muungano wa madaktari duniani na shirika la misaada la kikatoliki Caritas, yametoa maelezo na kufahamisha matatizo na ugumu wa maisha wanayopitia wahamiaji katika eneo la Vintimille nchini Italia.
Mashirika hayo yalitoa wito kwa Italia kufungua milango ya mipakani na kuwapokea wahamiaji haraka iwezekanavyo.
Wakati huo huo, mashirika hayo pia yaliituhumu Ufaransa kutokana na kifo cha mhamiaji mmoja wa Eritrea aliyegongwa na lori wakati alipokuwa akikaribia kwenye mpaka wa Italia na Ufaransa.
Viongozi wa Ufaransa na Italia wamekuwa wakilaumiwa kwa kufumbia macho mzozo wa wahamiaji wanaotaabika katika eneo la Vintimille lililoko mpakani kutokana na ukosefu wa misaada.
Kulingana na kanuni za Umoja wa Ulaya, wahamiaji hao wanapaswa kubakia Italia na hapo awali Ufaransa iliwahi kurudisha maelfu ya wahamiaji Italia kwa kutumia mabasi na treni.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment