Image
Image

Maandamano ya wanafunzi kwenye jengo la ofisi ya rais yafanyika mjini Sao Paulo nchini Brazil

Wanafunzi kadhaa wameripotiwa kuvamia ofisi ya rais wa serikali ya mpito katika mji wa Sao Paulo nchini Brazil Michel Temer aliyechukuwa nafasi ya Dilma Rousseff baada ya kung'olewa madarakani.Wanafunzi hao walitekeleza uvamizi wa ofisi ya rais Temer kwa lengo la kufanya maandamano ya kupinga kanuni ya matumizi ya fedha za serikali inayotambulika kama PEC 241.
Baadhi ya wabunge wa serikali pia wanaarifiwa kujiunga na kuwaunga mkono wanafunzi kwenye maandamano hayo.
Polisi walizunguka jengo la ofisi ya rais baada ya uvamizi huo ambapo kundi la mawakili na wabunge wa chama cha wafanyakazi cha PT wakiongozwa na Marcia Lia na Alencar Santana Braga walitangaza kuwaunga mkono wanafunzi kupinga kanuni hiyo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment