Chama
cha ACT- Wazalendo kimepanga kuwasha moto mjadala wa Katiba mpya katika
mkutano wake kidemokrasia kilioitisha jijini Dar es Salaam Oktoba 8.
Mkutano
huo unalenga kufufua mchakato wa Katiba Mpya kwa kuzingatia michakato
ya katiba za nchi nyingine za Afrika, alisema Katibu wa itikadi na
uenezi wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu alipozungumza na waandishi jijini
Dar es Salaam jana.
Alisema katika kupata uzoefu, ACT Wazalendo
imemualika Adabu Namwamba, ambaye ni kiongozi wa Chama cha Labour cha
Kenya kilichofanikiwa kubadilisha katiba yake baada ya mchakato mrefu.
Aliwataja
wageni wengine kuwa ni mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania, Deus
Kibamba ambaye naye atatoa mada kuhusu suala hilo.
Mchakato wa
kuandika Katiba mpya nchini umekwama katika hatua ya kupiga Kura ya
Maoni baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kushindwa kukamilisha
uandikishaji wapigakura kwa muda uliotakiwa.
Mchakato huo uligubikwa
na vikwazo kadhaa, ikiwa ni pamoja na vyama vinne vya upinzani na
baadhi ya wajumbe kususia kwa maelezo kuwa Bunge liliacha Rasimu ya
Katiba iliyokuwa na maoni ya wananchi na kuingiza sera za CCM.
Katika mkutano huo, kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe atawasilisha mada kuhusu hali ya nchi kwa mtazamo wa chama hicho.
“Kiongozi
wetu atawasilisha uchambuzi mpana wa kina zaidi kuhusu hali ya nchi
yetu kiuchumi, kisiasa na kijamii tangu Serikali ya Awamu ya Tano
ilipoingia madarakani,” alisema.
Pia, mwenyekiti wa ACT Wazalendo,
Anna Mghwira, ambaye aligombea urais mwaka jana, ataeleza uzoefu wake
katika uchaguzi, wakati mshauri wa chama hicho, Profesa Kitila Mkumbo
atachambua mwelekeo wa chama hadi mwaka 2020.
“Chama kinatoa wito kwa wananchi wanaotaka kushiriki katika mkutano huo kuwasiliana na ofisi ili kujiandikisha,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment