Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa amewasili jana
jioni katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na
kupokelewa na Mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Samia Suluhu Hassan jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa atafanya ziara ya kikazi ya
siku Tatu hapa nchini na lengo la ziara hiyo ni kuendeleza na
kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Cuba katika sekta mbalimbali
ikiwemo elimu,afya, utamaduni,michezo,kilimo, nishati, teknolojia na
kuangalia maeneo mapya ya uwekezaji.
Tarehe 3/09/2016 Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Cuba atakutana na kufanya mazungumzo ya faragha na Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli ikulu jijini Dar es
salaam.
Makamu wa Rais huyo wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio
Valdes Mesa pia atakutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ikulu na baada ya
mazungumzo hayo ya faradha viongozi hao watafanya mkutano na waandishi
wa habari kuzungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi
hizo mbili
Nchi nyingine ambazo Makamu wa Rais huyo wa Jamhuri ya
Cuba anazitembelea ni Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo-
DRC-,Botwana na Zimbabwe.
Home
News
Slider
Makamu wa Rais wa Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa awasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku Tatu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment