Mtu mmoja ameripotiwa kupewa hukumu ya kifungo
cha mwaka mmoja na miezi sita gerezani kwa madai ya kumtishia maisha
waziri mkuu wa Ujerumani Angela Merkel kwenye mtandao wa jamii.Mtu
huyo anayeishi mjini Würzburg anadaiwa kukumbwa na kizaazaa hicho baada
ya kuandika ujumbe mtandaoni na kubainisha nia yake ya kutaka kumpiga
risasi Merkel.
Mtu huyo aliyetoa kauli za kibaguzi, aliarifu kuandika ujumbe huo kwa kudai kuwa Merkel na viongozi wenzie wa Ujerumani ni wahaini wa taifa.
Katika ujumbe wake, mtu huyo mwenye umri wa miaka 31 pia alitaka kambi ya Auschwitz iliyokuwa ikitumika kwa mauaji ya halaiki wakati wa utawala wa Nazi.
Mtuhumiwa huyo anadaiwa kuwahi kumtishia Merkel hapo awali na hukumu yake ya kifungo cha gerezani ikaondolewa.

0 comments:
Post a Comment