Image
Image

Watoto pacha walioungana kichwa wafanyiwa upasuaji na kutenganishwa nchini Marekani.

Watoto wawili pacha walioungana kichwa wameweza kufanyiwa upasuaji na kutenganishwa kwa mafanikio nchini Marekani.Watoto hao pacha Anias na Jadon McDonald, walifanyiwa upasuaji uliodumu kwa masaa 27 katika hospitali moja ya kuu ya Montefiore iliyoko mjini New York.
Madaktari waliohusika na upasuaji walitumia masaa 16 kuwatenganishwa watoto hao na baadaye masaa mengine 9 kuziba utosi wa vichwa vyao.
Shughuli ya upasuaji wa watoto hao pacha imegharimu fedha zaidi ya dola elfu 100.
Nicole McDonald ambaye ni mama wa watoto hao aliandika ujumbe kwenye mtandao wa jamii wa Facebook na kutoa shukani za dhati kwa mafanikio ya upasuaji huo licha ya kuwa na hofu kubwa hapo awali kuhusu maisha ya baadaye ya wanawe.
Wataalamu wamebainisha kwamba asilimia 80 ya watoto pacha wanaozaliwa wakiwa wameugana viungo vya mwili hufariki baada ya kuishi kwa miaka miwili pekee.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment