Chama cha SDPK kilichokuwa kwenye serikali ya muungano nchini Kirgizistan kimetangaza kuchukuwa uamuzi wa kujiondoa uongozini.Kufuatia uamuzi huo, waziri mkuu Sooronbay Ceenbekov wa serikali ya muungano amewasilisha barua ya kuvunjika kwa serikali hiyo.
Rais wa Kirgizistan Almazbek Atambayev ameidhinisha uamuzi wa kuvunjwa kwa serikali hiyo ya muungano iliyoundwa na vyama vinne vya kisiasa mwezi Aprili.
Katika maelezo yaliyotolewa na ofisi ya rais, iliarifiwa kwamba Sooronbay Ceenbekov pamoja na wanachama wenzie wataendelea kuhudumu hadi serikali mpya itakapoundwa.
Uamuzi huo wa kujiondoa kwenye serikali ya muungano unaarifiwa kuchukuliwa kutokana na ukosefu wa maelewano katika suala la marekebisho ya katiba kati ya vyama vya kisiasa.

0 comments:
Post a Comment