Chama
cha Wananchi (CUF) kanda ya Kusini inayojumuisha mikoa ya Lindi na
Mtwara,kupitia wajumbe wa Baraza kuu la uongozi Taifa,kimetangaza
kutomtambua Profesa Ibrahimu Haruna Lipumba,kama kiongozi halali wa
Chama hicho.
Azimio hilo limetolewa na wajumbe hao pamoja na baadhi
ya wadhamini wa Chama hicho, baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati
tendaji ya kanda hiyoambacho kimefanyika kwenye Ofisi ya CUF iliyopo
mtaa wa Msonobarini Manispaa ya Lindi.
Akitangaza azimio hilo kwa
niaba ya wajumbe wa kikao hicho,Mwenyekiti wa CUF Lindi Salum Bar’wani
ametaja sababu mbalimbali ambazo zimewafanya wafikie uamuzi huo kama
vile kitendo cha Profesa kujiuzuru Uongozi wakati uchaguzi Mkuu
unaendelea,pamoja na kutekeleza maamuzi halali ambayo yametolewa na
uongozi wa Baraza kuu la Chama hicho kwenye kikao kilichofanyika
Zanzibar,na pia ametumia nafasi hiyo kukanusha taarifa zinazodai kuwa
CUF Kanda ya Kusini inamwunga mkono Profesa Lipumba.
Miongoni mwa
watu ambao wamehudhuria Mkutano huo ni Mdhamini wa Chama Abdalah Khatau
kutoka Masasi,pamoja na wabunge Ahmad Khatani wa Jimbo la Tandahimba
mkoani Mtwara na Seleman Bungara kutoka Jimbo la uchaguzi la Kilwa
Kusini Mkoani Lindi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment