Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limeutaka uongozi wa klabu ya Yanga kuwasilisha mkataba wa kukodishwa kwa kipindi cha miaka kumi ilioingia na kampuni ya Yanga Yetu Limited.
Wiki iliyopita bodi ya wadhamini ya Yanga ilitangaza kuwa itakodishwa kwa kipindi cha miaka kumi huku ikiainisha vipengele mbalimbali vilivyomo ndani ya mkataba huo.
Akizungumza na waandishi wa habari Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine amesema amemuandikia barua kaimu katibu mkuu wa Yanga kuomba nakala ya mkataba huo.
"Katika uendeshaji wa soka tunatambua suala la uwekezaji lakini ni lazima uzingatie kanuni na taratibu zilizowekwa.Tumesikia Yanga wamesaini mkataba wa kukodishwa. Tumepata barua za malalamiko mbalimbali ya wanachama na wazee wakihoji uamuzi huo,” alisema Selestine.
0 comments:
Post a Comment