Waasi 10 wa Uganda wameripotiwa kupewa hukumu ya kifo nchini DRC kwa madai ya ukiukaji wa haki za kibinadamu.Msemaji
wa serikali ya DRC Lambert Mende ametoa maelezo na kuarifu kukamatwa
kwa waasi hao kwenye operesheni iliyoendeshwa na jeshi nchini humo.
Mwezi uliopita, waasi wengine 10 pia waliwahi kukamatwa na kuhukumiwa kifo na mahakama ya kijeshi ya Beni nchini DRC.
Kwa sasa mahakama pia inatarajiwa kutoa hukumu kwa waasi wengine 80 waliokuwa kizuizini.
Waasi wa Uganda wamekuwa wakiendesha mashambulizi ya mara kwa mara tangu mwaka 1986 baada ya kuanza kuipinga serikali ya rais Yoweri Museveni na baadaye kujumuishwa kwenye orodha ya UN ya makundi ya kigaidi.
Kwa kipindi cha miaka 20 wanajeshi wa DRC wakishirikiana na kikosi cha UN cha kulinda amani cha MONUSCO wamekuwa wakiendesha operesheni dhidi ya waasi hao.
Kulingana na takwimu za mashirika ya umma, takriban raia 1,200 wamepoteza maisha kwenye mashambulizi ya waasi tangu mwezi Oktoba 2014 hadi kufikia sasa.

0 comments:
Post a Comment