Idadi ya vifo kufuatia kimbunga Matthew nchini Haiti inakaribia watu 300, kwa mujibu wa serikali.
Katika Mji wa Jeremie asilimia 80 ya majengo yameporomoka.
Hadhi
ya Kimbunga Matthew kwa mara nyingine imepandishwa hadi ngazi ya nne,
hatua ambayo ndiyo ya pili kwa ukubwa katika mgawanyo wa aina mbali
mbali za Kimbunga, huku kikielekea katika jimbo la Florida nchini
Marekani.
Maafisa wa serikali ya Haiti wametoa takwimu mpya kuhusiana na maafa yaliyosababisha na kimbunga hicho.
Siku ya alhamisi, serikali ya nchi hiyo ilisema watu mia moja tayari walikuwa wamepoteza maisha yao.
Kimbunga
Matthew ambacho ndicho kubwa zaidi katika visiwa vya Caribbean kwa
zaidi ya muongo mmoja uliopita, kimepiga taifa la Bahamas baada ya
kupitia Haiti na Cuba.
Wengi wa waliopoteza maisha nchini Haiti,
walikuwa wakiishi mjini na vijiji vinavyojulikana kwa shughuli za uvuvi
katika maeneo ya pwani ya kusini.
Wengi walifariki baada ya
kuangukiwa na miti, taka zilizokuwa zikisombwa au hata kusombwa na maji,
baada ya mito nyingi kuvunja kingo zao.
Kimbunga hicho kiliambatana na upepo uliokuwa ukivuma kwa kasi ya hadi kilomita 280 kwa saa.
Usafiri
kati ya maeneo ya kusini Magharibi na meneo mengine nchini Haiti
ulisitishwa baada ya daraja moja muhimu inayounganisha maeneo hayo
kusomba na maji.
Mashirika yasiyo ya kiserikali yamesema kwa sasa
hakuna huduma za simu na umeme na kuwa watu wanapungukiwa na vyakula na
maji safi ya kunywa.
Mratibu wa umoja wa mataifa anayehusika na
masuala ya misaada ya kibinadam amesema kuwa zaidi ya watu laki tatu na
nusu wanahitaji misaada ya kibinadamu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)









0 comments:
Post a Comment