Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa
ameuagiza uongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA),
kuhakikisha wanaweka mipango madhubuti ya kuongeza mapato katika vivuko
vya MV. Kigamboni na MV. Magogoni kutoka Shilingi Milioni 14 ambazo
zinakusanywa hivi sasa hadi kufikia Milioni 19 kwa siku.
Akizungumza jijini Dar es Salaam mara baada ya kukagua vivuko hivyo na
kuongea na Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dk. Mussa Mgwatu, Profesa Mbarawa
alisema kuwa kipimo cha utendaji huo utafanyika ndani ya miezi minne ili
kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wa vivuko hivyo na kuweza kufikia
malengo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)



0 comments:
Post a Comment