Image
Image

Mfalme wa Morocco kufanya ziara ya kihistoria nchini Tanzania.

KWA mara ya kwanza katika historia yake, Tanzania inatarajia kumpokea Mfalme Mohammed wa VI wa Morocco keshokutwa. Aidha, ziara ya mfalme huyo, mbali na kujikita katika kujenga diplomasia ya nchi hizo mbili, itatumika pia kuiomba Tanzania kusaidia kupokewa kwa Morocco katika Umoja wa Nchi za Afrika (AU).
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk Augustine Mahiga alisema ugeni huo utakuwa mkubwa na wa aina yake.
“Sababu mbili za ziara hii ya mfalme hapa nchini ni Morocco ilijiondoa katika Umoja wa Nchi za Afrika miaka 32 iliyopita, lakini hivi karibuni wanachama walipokea barua kutoka kwa nchi hiyo kutaka kurudi katika umoja huo, kwa kuja hapa atazungumza na Rais,” alisema Balozi Mahiga.
Mfalme Mohammed wa VI atakutana kwa mazungumzo ya faragha na Rais John Magufuli Ikulu yakifuatiwa na mazungumzo rasmi kati yao na ujumbe aliofuatana nao. Balozi Mahiga alisema mfalme huyo atakuja nchini akitokea Rwanda, na atakuwa na ziara ya kutembelea nchi nyingine Afrika kuzungumza nao kuhusu kurudi kwake AU.
Alisema ziara hiyo pia itatumika kukuza zaidi uhusiano kati ya Tanzania na Morocco hususan katika masuala ya kiuchumi na kibiashara kwa faida ya nchi hizi mbili na watu wake ikizingatiwa nchi hiyo imefanikiwa sana katika nyanja mbalimbali kama vile miundombinu, afya, madini na ulinzi.
Waziri huyo alifafanua kuwa ziara rasmi nchini ya mfalme itakuwa kuanzia Jumapili hadi Oktoba 25, mwaka huu na baada ya hapo atakuwa likizo kwa siku tano ambapo atatembelea sehemu mbalimbali kama matembezi binafsi.
Vilevile, alisema Mfalme Mohammed wa VI wa Morocco atatumia fursa ya ziara hiyo kutembelea Zanzibar na kukutana na Rais Ali Mohamed Shein na atatembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCCA) kwa ajili ya kujionea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
Ziara hiyo ambayo imejikita zaidi katika kukuza ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara, ujio wa mfalme atafuatana na wafanyabiashara kutoka Morocco ambao watakutana na wafanyabiashara wa nchini.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment