WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema hadi
kufikia mwaka 2025, sekta ya madini nchini inapaswa ichangie asilimia 10
kwenye Pato la Taifa.
Katika kipindi cha mwaka 2015 sekta hiyo imechangia asilimia 4.3
kutoka asilimia 3.7 kwa mwaka 2014, kiasi ambacho waziri huyo amesema
bado ni kidogo.
Aliyasema hayo mjini Dodoma jana mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Nishati na Madini wakati akitoa taarifa kuhusu shughuli za utafutaji
madini na maendeleo ya sekta ya madini.
Hata hivyo, alitaja changamoto zinazoifanya sekta hiyo kuwa na
mchango mdogo katika Pato la Taifa kuwa ni pamoja na kushuka kwa bei ya
madini kwenye soko la dunia na kutokuanzishwa kwa migodi mingine mikubwa
ya uchimbaji hivi karibuni.
Alisema kwa sasa uwezo wa uzalishaji wa dhahabu kwa migodi yote
nchini ni wakia milioni 1.25 kwa mwaka na uzalishaji kuanzia mwaka 2011
hadi 2015 ni wakia milioni 5.68 sawa na tani 176.7 yenye thamani ya dola
za Marekani bilioni 9.06 sawa na Sh trilioni 19.7.
Waziri huyo alifafanua kuwa ipo mipango mbalimbali ya kuendeleza
shughuli za madini nchini ikiwemo kuboresha ukusanyaji na usambazaji wa
taarifa na takwimu za kijiosayansi, udhibiti wa utoroshwaji wa madini na
ukaguzi katika shughuli za uzalishaji madini.
Naye Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche alitaka kujua hatua
zinazochukuliwa dhidi ya tuhuma za utoroshaji wa madini unaofanyika
katika baadhi ya migodi ikiwemo mgodi wa Accacia ambao ndani ya mgodi
kuna kiwanja cha ndege.
Home
News
Slider
Muhongo: Kufikia 2025, sekta ya madini nchini inapaswa ichangie asilimia 10 kwenye Pato la Taifa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment