Wakati
Donald Trump na Hillary Clinton walipokwea jukwaani St Louis kwa
mjadala wa pili kati ya mitatu iliyopangwa, hakupeana salamu kwa mikono ,
jambo lililodhihirisha chuki ambayo ingeendelea katika kipindi kizima
cha mjadala huo.
Donald Trump ametangualia kwa kutetea matusi
aliyotoa kuhusu kuwagusa wanawake katika sehemu za siri kwa kumshambulia
Hillary Clinton na mumewe.
Mgombea huyo wa chama cha Republican,
amekana kamwe hajawanyanyasa wanawake kingono, lakini akageuza hasira
kwa aliyekuwa rais wa Marekani Bill Clinton katika majibizano makali
kwenye mjadala huo
"Hakuna mtu katika historia ya siasa ambaye amewanyanyasa wanawake kiasi hicho," alisema.
Hillary Clinton alikataa kujibu tuhuma hizo dhidi ya mumewe.
Matamshi
ya bwana Trump dhidi ya failia ya Clintons yalijiri baada ya muendesha
mjadala Anderson Cooper kumuuliza kuhusu kanda ya video ya mwaka 2005
iliyosambazwa katika vyombo vya habari Ijumaa iliyomfichua Trump
akijigamba kuhusu kuwagusa wanawake katika sehemu zao za siri.
Lakini
alipoendelea kuulizwa kuhusu iwapo alimnyanyasa kingono mwanamke
yoyote, alikana kufanya hivyo na badala yake akamulika tuhuma
zilizomuandamana Bill Clinton katika siku za nyuma.
Hakuna mashtaka ya uhalifu yaliowasilishwa dhidi ya Bwana Clinton katika tuhuma zozote z unyanyasaji wa kingono.
Wagombea
hao wawili bila walizozana kuhusu mzozo wa Syria, Uchokozi wa Urusi, na
hatua ya bwana Trump kukata kutangaza malipo yake ya kodi na mpango
wake wa ukaguzi mkali kwa wahamiaji wanaowasili kutoka mataifa
yanayohusishwana ugaidi.
Hatimaye mjadala ulikamilika wakati
mwanamume mmoja kutoka umati uliokusanyika kufuatilia mjadala huo,
alipowauliza wagombea hao wawili kusema kitu kimoja kizuri kumhusu
mwenzake.
Mgombea wa chama cha Democrat Hillary Clinton akasema watoto wake Trump wanamdhihirisha ni mtu wa aina gani.
Naye Trump akamtaja mpinzani wake kuwa "mpiganaji" asiye kata tamaa.
Home
Kimataifa
Slider
Mjadala wa urais Marekani: Trump vs Clinton wachuniana kupeana salam na kuanza kushambuliana.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment