KLABU ya Simba imesema kwamba imechoshwa na danadana za Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF) kuhusu hatma ya suala la beki wao, Hassan Ramadhani
Kessy, ambaye amesajiliwa na mahasimu wao, Yanga, kinyume cha sheria.
Kwa mujibu wa mitandao ya kijamii jana, Mwenyekiti Kamati ya Usajili
ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe alisema kwamba mara ya mwisho TFF
iliwaambia suala hilo lingemalizwa ndani ya mwezi uliopita, lakini sasa
ni Oktoba na bado halijamlizika.
Alisema kwamba katika kikao cha mwisho walikubaliana na Yanga
kuwaomba Mawakili Said El Maamry na Profesa Mgongo Fimbo kuwasimamia
katika kutafuta suluhisho la suala hilo.
Sheria na Hadhi za Wachezaji ku wapa siku tatu kuanzia Septemba 24,
2016 kumaliza wenyewe suala hilo, hatua ambayo ilifikiwa baada ya
mjadala wa muda mrefu kuhusu kesi mbili zilizofunguliwa na Simba mbele
ya kamati hiyo inayoongozwa na Mwanasheria Richard Sinamtwa.
Kesi hizo ni Yanga kudaiwa kuingia mkataba na Kessy wakati bado ana
mkataba na Simba na ya pili ni mchezaji huyo kudaiwa kuanza kufanya
mazoezi bila kusajili Yanga na kwenda nje ya nchi wakati akiwa ndani ya
klabu yake hiyo ya zamani.
Poppe alisema kwamba kwa sababu tangu wiki iliyopita wamekuwa
wakipigwa danadana na TFF na Yanga juu ya suala hilo, wanaona bora
lirudishwe kwenye Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji
limalizwe huko.
Wakati inatoa agizo la kuzitaka klabu hizo zimalizane zenyewe, Kamati
ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ilisema kwamba kama hawatafikia
muafaka katika siku tatu walizopewa, mashauri hayo yatarudi mbele ya
kamati na kufanya uamuzi kwa mujibu wataratibu, kanuni na sheria
zinazoongoza mpira wa miguu Tanzania.
Ikumbukwe katika madai yake, Simba inataka ilipwe dola za Kimarekani 600,000 zaidi ya Sh bilioni 1.2 za Tanzania.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment