MUUGUZI wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru,
Scolastica Leoni (43) ambaye ni mkazi wa kata ya Sanawari amepandishwa
kizimbani kujibu shitaka moja la kuiba mtoto mchanga wa kiume wa siku
nne.
Akisomewa mashitaka na Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Pennina
Joackim mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Arusha, Patricia
Kisinda, ilidaiwa mshtakiwa alifanya kosa hilo Aprili 15, mwaka huu
majira ya usiku wa manane akiwa kazini.
Mwendesha Mashitaka alidai kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo akiwa
kazini katika Hospitali ya Mount Meru wakati akifahamu wazi kufanya
hivyo ni kosa kisheria na ni kinyume cha sheria na kanuni na taratibu za
kazi. Alidai muuguzi huyo akiwa mtumishi wa umma katika hospitali hiyo
aliiba mtoto muda mfupi baada ya kuzaliwa.
Alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume cha Kifungu 169 kifungu
kidogo cha 1(a) cha Sheria na Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 kama
ilivyofanyiwa marekebisho 2002.
Mshtakiwa alikana shitaka na hakimu alisema dhamana ni haki ya mtu
kwa mujibu wa sheria hivyo anatakiwa kudhaminiwa na wadhamini wawili
wenye mali isiyohamishika yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 20.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment