Dar es Salaam. Rais
John Magufuli anaongoza kura za kuwania tuzo ya ‘Forbes Africa Person
of The Year’, ambayo hutolewa kwa watu walioonyesha mchango kwa jamii.
Huku
zikiwa zimebaki siku 21 kwa mshindi wa tuzo hiyo kutangazwa, Rais
Magufuli anachuana na Rais wa Mauritius, Ameenah Gulib; Mwendesha
Mashtaka wa Afrika Kusini, Thuli Madonsela; Mwanzilishi wa Capitec Bank,
Michiel Le Roux na Taifa la Rwanda.
Mpaka
jana jioni, Dk Magufuli alikuwa anaongoza kwa asilimia 75 likifuata
Taifa la Rwanda na nafasi ya tatu alikuwa Madonsela wa Afrika Kusini.
Rais
Magufuli anayetimiza mwaka mmoja madarakani wiki ijayo, utendaji wake
umeonekana kuwagusa wananchi wa kipato cha chini, hasa kwa falsafa yake
ya Hapa Kazi, uwajibishaji na mikakati yake ya kubana matumizi ili
kuokoa fedha kwa kuzuia sherehe zisizo na tija.
0 comments:
Post a Comment