RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein anatarajiwa kufungua mkutano wa kikako cha tano cha Bunge la
Afrika Mashariki (EALA) utakaoanza leo visiwani hapa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Unguja, Spika wa Bunge
la Afrika Mashariki, Daniel Kidega alisema kikao hicho kitajadili na
kupitisha miswaada mitatu.
Alisema miswaada hiyo ni ile ya usawa wa kijinsia na maendeleo kwa
nchi za EAC, uzuiaji wa usafirishaji haramu wa binadamu vitendo ambavyo
vimekithiri katika miaka ya hivi karibuni.
“Kama tunavyojua suala la biashara haramu ya binaadamu ipo katika
nchi mbali mbali na wananchi wengi wanatoka katika nchi za Afrika
Mashariki na kwenda nchi za Ulaya kwa hivyo hili nayo linahitaji
kujadiliwa kwa kina” alisema Spika Kidega
Alisema suala hilo linahitaji mjadala mpana kutokana na uzito wake na
hivyo wabunge wa bunge hilo watajadili na kuona namna gani ya
kukabiliana na changamoto iliyopo juu ya biashara hiyo ambayo inapaswa
kushughuulikiwa na kuwekewa mikakati madhubuti.
Kwa upande wake Mbunge wa Bunge hilo kutoka Tanzania, Makongoro
Nyerere, alisema ni utaratibu wa kawaida wa EALA kufanya vikao vyake
katika nchi za Afrika Mashariki ambapo Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Home
News
Slider
Shein anatarajiwa kufungua mkutano wa kikako cha tano cha Bunge la Afrika Mashariki (EALA)
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment