Wakati Serikali ikitanfaza msako kwa watu walioghushi vyeti na
kutumia majina ya watu wengine, Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi,
Mwigilu Nchemba, ameibuka na kutoa ufafanuzi wa utata wa majina yake.
Hatua hiyo imekuja baada ya kuibuka kwa mjadala wa usahihi wa majina yake pamoja na kuhusishwa kughushi vyeti ya elimu.
Katika andiko lake aliloliweka jana katika mitandao ya kijamii ambalo
baadaye lilithibitishwa na mmoja wa wasaidizi wake, Mwigulu alisema
watu wanaoandika historia yake hawamjui kwani uhalisia alikuwa akiitwa
Lameck Madelu Mkumbo, sasa Lameck si jina la Kinyiramba na Madelu si
jina halisi la baba yake bali la utani.
“Ni vema kuweka rekodi sawa, kwanza anasema (aliyeandika) nilikuwa
naitwa Lameck Madelu Mkumbo, sasa moja Lameck sio jina la kinyiramba, na
Madelu sio jina halisi la baba bali ni utani kuwa ana ndevu nyingi,
yaani ni mandevu. Ndiyo maana hata kwenye ubunge nililiongeza tu kama
a.k.a ili watu, hasa wazee wanifahamu, hili haliko kwenye vyeti.
“Hili la Lameck siyo jina la Kinyiramba ni jina la daktari
aliyenipokea zahanati iliyopo Kijiji cha Mukulu, daktari tunaita hivyo,
lakini ni nesi ndiye aliyekuwa anaitwa Mwigulu na jina la kizungu
Lameck.
“Mimi nilipelekwa hospitali nikiitwa Mugulo na jina la ukoo kwa
watoto wote wa kiume ni Shumbi, ambalo hata hivyo wanatumia wazee tu,
wanaojua Kinyiramba hilo ndio jina la Kinyiramba,” alisema Mwigulu na
kuongeza:
“Mama yangu aliulizwa jina akanitaja kwa muuguzi (nesi) akamwambia
mama unamwitaje jina hilo hakuna lingine, mama akamwambia hakuna labda
mtaje wewe, basi jamaa akajitaja,” alisema.
Alisema suala hilo ni jambo la kawadai hasa kwa kijijini kwani
familia inakuwa na watoto wengi hadi majina inakuwa si jambo la kujali.
“Hata pale kijijini kuna wengine waliotajwa majina ya waganga wa
kienyeji wazee walikopewa dawa, majina ya manesi, matabibu kama mimi,
majina ya walimu,” alisema.
Akizungumzia maisha yake ya elimu, alisema aliacha shule kwa mara ya
kwanza mwaka 1984 baada ya kuanza na kaka yake aliyemtaja kwa jina la
Jugulu.
Mbunge huyo wa Iramba alisema kutokana na hali hiyo, baba yao
aliwataka wapeane zamu ya kwenda shule hali iliyomfanya aache shule.
“Mwaka 1985, nikaachia darasa la tano nikaenda kuchunga miaka kama
miwili. Nikarudi tena baada ya mifugo kuanza kufa sana, mzee akashauriwa
awekeze kwenye elimu. Walimu walikuwa wanashinda nyumbani kumsihi
anirudishe shule, ndiyo nikarudi na nikachukua majina ya daktari.
“Mtu asichanganye kuona ni udanganyifu, mimi sijachukua vyeti vya
mtu. Nimefanya mitihani tena kwa kupiga na picha za passport ili mtu
asitumie haki ya mtu mwingine aliyefaulu na mpaka sasa naona ni struggle
(kupambana) za mfano, kuwa nilisoma kwa mazingira ya kutoka kuchunga na
kurudishwa shule na kufaulu mwenyewe,” alisema Mwigulu.
Waziri huyo alisema kwa anayetaka kuthibitisha maelezo aliyotoa, anaweza kuwauliza aliosoma nao shule ya msingi.
“Comrades kwa mawazo yangu kosa ni mtu kuchukua nafasi ya mtu
aliyefaulu na kwenda yeye, hapo ni kuiba haki ya mtu. Najua hii ilikuwa
ikitokea baadhi ya maeneo, mtu anafaulu ila anakuwa hataki kwenda shule
au amefariki then anakwenda mwingine. Mimi sijawahi chukua nafasi ya
mtu.
“Halafu watu wanasema jina la mtu, labda kama wanamaanisha tofauti na
wizi wa jina kwani kila mmoja hapo alipo ana jina la mtu, yaani atakuwa
John wa Biblia, Mohamed wa Quran, litakuwa la babu, bibi la mganga,
daktari, rafiki, kiongozi au hata la tukio.
“Nijuavyo jina unakula kiapo tu kama sio la kwako kisheria na
unatumia, na hata sasa nikitamani jina jipya nakula kiapo na kutangaza
katika Gazeti la Serikali na lisipopingwa ndiyo linakuwa jina langu
jipya.
“Hoja ni kama mtu kapora cheti cha mtu, kapora nafasi ya mtu mwingine
aliyefaulu akaenda kuisomea yeye. But, things do change pia kutokana na
nyakati na mazingira,” alisema Mwigulu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment