Zitto Kabwe (Juu), Mrisho Gambo (Kushoto) na Godbless Lema (chini kulia)
Mbunge
wa Kigoma Mjini kupitia tiketi ya ACT Wazalendo Zitto Kabwe
amesikitishwa na kitendo cha kutoelewana kikazi kati ya Mkuu wa Mkoa wa
Arusha Mrisho Gambo na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema.
Zitto
kupitia ukurasa wake wa facebook amesema anakasirishwa sana kuona
viongozi wanafanya mambo ya hovyo jambo ambalo litafanya vijana
washindwe kuaminiwa katika nafasi wanazopewa kwa kutotumia hekima na
busara katika majukumu yao.
“Nakasirishwa sana kuona viongozi
vijana wanafanya mambo ya hovyo. Mkuu wa Mkoa wa Arusha mdogo wangu
Mrisho Gambo una dhamana zaidi kwa vijana. mnapofanya mambo ya kijinga
mnaharibu nafasi ya vijana kuaminiwa zaidi” Amesema Zitto.
Aidha
Zitto amemtaka Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kupunguza munkari
katika majukumu yake kwani mchango wake kwa wananchi wa Arusha hauwezi
kufutika kirahisi.
Pamoja na hayo Zitto amewashauri viongozi hao
kukaa pamoja meza moja na kujenga Arusha na kuacha kuonesha hasira zao
hadharani kwa wananchi.
Kauli ya Zitto imefuatia kutokuwepo kwa
maelewano ya mara kwa mara baina ya viongozi hao ikiwemo tukio la jana
la Mbunge Lema kutofautiana na Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo hadharani
wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment