Image
Image

Coaster yaua 4 yajeruhi zaidi ya 20 jijini Mbeya.

Watu 4 wamepoteza maisha na wengine 22 kujeruhiwa baada ya basi dogo la abiria aina ya Coaster linalofanya safari zake Mbeya na Chunya kupinduka katika Kijiji cha Majimazuri, Wilaya ya Mbeya Vijijini katika Barabara ya Mbeya/Chunya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashari amesema kuwa ajali hiyo imetokea mnamo tarehe 18.10.2016 majira ya saa 9:50 Alasiri ikihusisha gari lenye namba za usajili T.841 BRW aina ya Isuzu basi likitokea Wilaya ya Chunya kwenda Mbeya.
Amesema gari hilo lililokuwa likiendeshwa likiendeshwa na dereva aitwaye ELIA ISACK [37] Mkazi wa Chunya liliacha njia, kupinduka na kusababisha vifo kwa abiria wanne ambao ni HAWA MOHAMED [30] mkazi wa Chunya, Mtoto mdogo wa miaka 2 wa kiume ambaye bado kufahamika jina lake na wanaume wawili ambao hawakufahamika majina yao.
Amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na kwamba majeruhi wote wamelazwa Hospitali ya Rufaa Mbeya na dereva amekamatwa huku upelelezi ukiwa bado unaendelea.
Aidha katika ajali abiria 22 walijeruhiwa kati yao wanawake 14 na wanaume 08.
Majeruhi walitambulika kwa majina ya

1. HAPPY BAKARI [28] Mkazi wa Mabatini
2. FAIDA MBUYI [47] mkazi wa Igodima
3. AGNESS LUSUPA [45] Mkazi wa Ileje
4. EMMY MWASIMBIHABI [35] Mkazi wa Mwakaleli
5. LONGI MWALUVANDA [45] Mkazi wa Chunya
6. SIWANGU PAUL [28] Mkazi wa Simike
7. RODA GUNZA [38] Mkazi wa Chunya
8. ANITHA FRANK [18] Mkazi wa Igodima
9. MAGDALENA ALMASI [19] Mkazi wa Iganzo
10. AGNESS NDOKILE [38] Mkazi wa Iganzo
11. ELIZA GIDION [21] Mkazi wa Chunya
12. JULIANA MWAMPASHI [36] Mkazi wa Chunya
13. SARAH ENOCK umri wa mwaka mmoja na nusu Mkazi wa Chunya na
14. EMMA ANGETILE [35] Mkazi wa Chunya.
Majeruhi wengine ni 1. MOSES JACKSON [29] Mkazi wa Itaka 2. JOHNPHANCE SAMSON [35] Mkazi wa Mbozi 3. PETRO LYANGA [24] Mkazi wa Tunduma 4. ISSA KALINGA [18] Mkazi wa Chunya 5. RICHARD KIHAMI mkazi wa Chunya 6. STARD MWASHITETE [34] Mkazi wa Mbozi 7. MWANDALIMA JOSEPH miaka kati ya 35 – 40 na 8. CHEYO NDELE [32] Mkazi wa Mbeya.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment