Image
Image

13 wafariki kwenye mkasa wa moto uliotokea ndani ya ukumbi wa burudani nchini Vietnam

Watu 13 wameripotiwa kupoteza maisha kufuatia mkasa wa moto uliozuka ndani ya ukumbi wa burudani ulioko katika mji mkuu wa Hanoi nchini Vietnam.Kulingana na taarifa zilizotolewa na gazeti la VnExpress, mkasa huo wa moto umearifiwa kuzuka hapo jana nyakati za usiku katika ukumbi huo ulioko juu ya ghorofa ya 8 ya jengo la mtaa wa Cau Giay.
Moto huo ulienea kwa kasi ndani ya muda mfupi na kuteketeza majengo mengine yaliyoko karibu na ukumbi huo.
Watu wengine wengi wakiwemo maafisa 2 wa polisi pia wameripotiwa kujeruhiwa kwenye tukio hilo.
Timu ya wazima moto ilifanikiwa kuudhibiti moto huo baada ya makabiliano yaliyodumu kwa masaa 5.
Waziri mkuu wa Vietnam Nguyen Xuan Phuc ametangaza kuanzisha uchunguzi ili kubainisha chanzo cha moto huo na kutoa wito wa kuimarisha usalama katika migahawa na kumbi za burudani kote nchini.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment