MAKAMU
wa Rais, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
mkutano wa wadau wa uendelezaji wa viwanda vya usindikaji utakaofanyika
Desemba 3 mwaka huu, jijini Dar es Salaam.
Hayo yalisemwa jana jijini
Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Chama cha Wasindikaji Tanzania (TAFOPA)
ambao ndio waandaaji wa mkutano huo wakati wakizungumza na waandishi wa
habari.
Licha ya Makamu wa Rais, viongozi mbalimbali wa serikali na binafsi wanatarajiwa kushiriki katika mkutano huo.
Alisema
lengo la mkutano huo ni kuzindua uanzishwaji na uendelezaji wa maeneo
ya viwanda vya usindikaji pamoja na kuhamasisha kutafuta washirika
kutoka katika mashirika ya kimataifa ili kwa pamoja wajadiliane jinsi
gani ya kuendeleza maeneo hayo ya usindikaji.
Aliongeza kuwa, chama
cha wasindikaji kwa kuliona hilo wameona ni muda muafaka kwa sababu
Tanzania inaelekea katika uchumi wa viwanda hivyo kupitia mkutano huo
utasaidia chama hicho kwa kushirikiana na wadau ili kutafuta maeneo ya
usindikaji na kuwaondoa kina mama kutoka kusindika majumbani na kuwa na
maeneo maalumu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment