MGANGA
wa kienyeji aliyejulikana kwa jina la Kashinje Kashinje (55), mkazi wa
kijiji cha Singita kilichopo Kata ya Usanda wilayani hapa ameuawa kwa
kupigwa na wananchi ikielezwa alijaribu kutaka kumbaka mteja wake.
Mteja huyo ambaye ni mwanamke mwenye umri wa miaka 20 (jina linahifadhiwa) aliyekwenda kutibiwa kwa lengo la kupata mtoto.
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Muliro Jumanne, tukio
hilo ni la Novemba 29 mwaka huu, akisema lilitokea majira ya saa tano
asubuhi.
Alisema Kashinje alifariki dunia alipokuwa anakimbizwa
hospitali baada ya kujeruhiwa kwa kitu chenye ncha kali katika jicho la
kulia na kupigwa kwa fimbo mgongoni na watu waliojichukulia sheria
mkononi.
“Watu hao walijichukulia sheria mkononi baada ya mganga huyo
kujaribu kumbaka mwanamke (jina linahifadhiwa), mkazi wa kijiji cha
Ishinabulandi wilaya ya Shinyanga ambaye alikuwa akimtibu kwa tiba za
asili ili aweze kupata mtoto”, alieleza kamanda Muliro.
Alisema tatizo lililompeleka mwanamke huyo kwa mganga ni kupata tiba ili aweze kupata mtoto.
Kamanda
Muliro alibainisha kuwa chanzo cha tukio hilo ni tamaa za kimwili na
uongo wa kimatibabu wa kutaka kumuingilia kimwili mgonjwa wake baada ya
kumlewesha kwa dawa za kienyeji, lakini alifanikiwa kupiga kelele na
ndipo wananchi walipomvamia mganga huyo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment