WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, amesema
Tanzania imeweka mazingira bora ya uwekezaji wa biashara kupitia Kituo
cha Uwekezaji nchini (TIC).
Akizungumza katika mkutano kati ya wafanyabiashara wa Tanzania na
Ubelgiji, jijini Dar es Salaam jana, Mwijage alisema kuwa mazingira
yaliyowekwa ni rafiki kwa uwekezaji katika maeneo mbalimbali ikiwemo ya
kilimo cha biashara.
Mwijage alisema kuwa Tanzania ni nchi inayokua kwa kasi duniani hivyo
wawekezaji wana nafasi ya kufanya uwekezaji kutokana na kuwa nchi ya
amani ambapo wanaweza kuwekeza na kuzalisha bila kuwepo kwa vikwazo.
Alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inapambana na rushwa ili
wananchi waishi bila rushwa, na kuyataja maeneo ya kufanya uwekezaji
yamepangwa katika maeneo ya biashara, kilimo, miundombinu, Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano (Tehama), madini, gesi, utalii na uvuvi.
Alisema kuna ushirikiano wa muda mrefu kati Tanzania na Ubelgiji
hivyo milango ya uwekezaji iko wazi na nchi nyingine zimeweka mikakati
ya uwekezaji.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment