Image
Image

Serikali yaombwa kuongeza maofisa ustawi wa jamii kukabiliana na ukatili katika jamii.

SERIKALI imeombwa kuongeza maofisa ustawi wa jamii ili kuongeza nguvu katika kuzishughulikia changamoto zinazotokea katika jamii hasa zinazohusu matukio ya ukatili kwa watoto.
Mwaka 2010, walikuwapo maofisa ustawi 108 kwenye mikoa na halmashauri, ingawa walitakiwa kuwapo wanane wenye shahada katika kila halmashauri na katika hospitali za wilaya walitakiwa kuwapo watano.
Akizungumza Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa tathmini ya kampeni ya miaka mitatu ya Nijali iliyokuwa ikiendeshwa na Shirika lisilo la Kiserikali la C-Sema, Mkurugenzi wa Miradi wa Shirika la SOS Arusha, Francis Msollo alisema bado kuna uhaba wa maofisa ustawi nchini.
Msollo alisema watoto wanahitaji malezi bora kuanzia nyumbani hadi katika jamii na watoto wasiopewa malezi bora ndio wanakuwa chanzo cha vikundi vya uhalifu wakiwamo ‘panya road’.
Mkurugenzi Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Rashed Maftah alisema pamoja na changamoto hiyo, lakini serikali imekuwa ikifanya jitihada za kuboresha mfumo na kuongeza idadi ya maofisa ustawi nchini kutoka 108 mwaka 2010 hadi 732 kwa sasa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment