Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May amempigia rais Recep Tayyıp Erdoğan na kutoa pole kwa janga la shambulizi la kigaidi jijini Istanbul.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya ofisi ya urais ni kuwa May alisema kuwa Uingereza ipo na Uturuki wakati huu mgumu na kuwapa pole hasa familia za wahanga wa shambulizi hilo.
Aidha Waziri huyo mkuu pia aliombea kupona kwa haraka kwa majeruhi katika mlipuko huo wa bomu.
Aliongezea kwa kusema kuwa amesikitishwa sana na shambulizi hilo na kutoa rambi rambi za dhati kwa rais Erdoğan na wananchi wa Uturuki kwa ujumla.
Home
Kimataifa
Slider
Recep Tayyıp Erdoğan apokea simu ya Theresa May ya pole kwa janga la shambulizi la kigaidi Istanbul.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment