Flora amebainisha hayo wakati akihojiwa na ENEWZ na hivyo kuweka wazi jina analotaka aitwe na mashabiki pamoja na jamii inayo mzunguka, huku akisema kuwa sasa anaamani na maisha anayo yaishi yenye upendo na furaha.
Amesema kwa sasa Maisha aliyojichagulia kuishi niyale ambayo yeye mwenyewe anayapenda kwani ni maisha ambayo hayaingiliani na mtu yeyote, nakusema kuwa hapendi kuyazungumzia sanaa katika vyombo vya habari kwakuwa hayapo kwaajili ya kuwanufaisha watu.
Hata hivyo Flora Mbasha alikuwaga na Msigano na Mumewe Mbasha katika mahusiano yao kutokana na sintofahamu ambayo wao walikuwa wakiifahamu mpaka kufikishana kwenye vyombo vya sheria na kutolewa maamuzi, Ambapo sasa Flora hakupenda kuzungumzia juu ya talaka nakusema kuwa 'swala la mahusiano na mapenzi ni ya watu wawili hivyo hataki kuweka wazi juu ya ishu yake ya kudai talaka'.
0 comments:
Post a Comment