Image
Image

Q-Chief asema vijana wanaotumia dawa za kulevya hawawezi kuacha bila kushindana na nafsi.


Mwanamuziki wa Bongo Flava nchini Tanzani Shaban Katwila almaarufu Q - Chifu amewaasa vijana wanaoingia katika utumiaji wa dawa za kulevya hawawezi kuacha kama hawataweza kushindana na nafsi zao.
Akizungumza kupitia Radio One Q-Chief amesema kuwa yeye alishatumia dawa za kulevya kwa makosa na akatambua hivyo nivema vijana kutambua kuwa dawa hizo hazina faida katika maisha, ambapo amewataka kujifunza kupitia kwake kwa mapitio aliyoyapitia.
Amesema kila mwanadamu mwenyezi mungu kamuandalia sehemu yake hivyo nivyema kijana kuondoa fikra za kufikiri za kutumia dawa na badala yake wafikirie kujenga maisha yatakayokuwa na manufaa hapo baadae.
Q-Chief amebainisha kwamba hajawahi kufikiri na wala hakufikiri kujihusisha na utumiaji wa dawa za kulevya kwa sababu za kushuka kimuziki bali aliingia tu kutokana na sababu zingine,ambapo kutokana na kuona alifanya makosa alijaribu kujinasua na utumiaji wa dawa hizo haswa kwa kuishirikisha nafsi yake kukataa utumiaji wa dawa hizo.


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment