Hali ya hatari ilitangazwa baada ya jaribio la mapinduzi lililotokea tarehe 15 Julai mwaka 2016.
Kwa kawaida hali ya hatari ingepaswa kuisha tarehe kumi na tano mwezi wa kwanza mwaka huu lakini mhula huu umeongezwa kwa siku tisini zaidi.
Numan Kurtulmuş amesema hii ni kwasababu serikali bado ina wasiwasi na kuwepo kwa wafuasi wa FETÖ katika vyombo mbalimbali vya serikali.
Hivyo basi Uturuki itazidi kusafisha nchi yake dhidi ya magaidi kwa miezi mitatu mingine.
Uturuki imekumbwa na misukosuko mingi sana ndani ya miaka michache iliyopita.
0 comments:
Post a Comment