Mkutano wa kwanza wa baraza la mawaziri ulifanyika Beştepe chini ya uongozi na usimamizi wa rais Recep Tayyıp Erdoğan.
Katika mkutano huo naibu waziri mkuu wa Uturuki Numan Kurtulmuş amefahamisha kuwa mshukiwa wa shambulizi katika ukumbi wa starehe mjini Istanbul anaanza kutambulika.
Katika mkutano huo kulizungumziwa kuhusu shambulizi la mjini Istanbuli katika ukumbi wa starehe mkesha wa mwaka mpya.
Numan Kurtulmuş katika hotuba yake amesema kuwa Uturuki haito salim amri mbele ya mashambulizi ya uhalifu.
Aliendelea kufahamisha kuwa Uturuki itaendelea kupambana na makundi ya kigaidi na kusema kuwa harakati za kusaka amani Mashariki ya Kati zitaendelea na Iraq inatarajiwa kuwa nchi salama.
Tunatambua ya kwamba operesheni na harakati zilizopelekea kutatua mzozo wa Syria na kuendelea na operesheni ya Fırat, makundi ya kşgaidi na washirika wake hawaridhishwi na kitendo hicho alizidi kufahamisha Numan Kurtulmuş.
0 comments:
Post a Comment