Polisi nchini Israel imesema kuwa imemuhoji Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, kuhusu madai ya kupokea zawadi kutoka kwa wafuasi na wafanyabiashara tofauti kinyume na sheria.
Benjamin Netanyahu alihojiwa saa zipatazo takribani tatu katika makazi yake mjini Jerusalem akituhumiwa kupokea "zawadi" kinyume na sheria.
Hakuna habari zaidi zilizotolewa kuhusu taarifa hiyo.
Wizara ya sheria pia imethibitisha katika taarifa yake kuwa Netanyahu alihojiwa na kitengo cha polisi ya kupambana dhidi ya rushwa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment