Watu saba wamekufa na wengine wanne wamejeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea eneo Mwika, mkoani Kilimanjaro.
Miongoni mwa waliofariki ni waandishi wawili wa habari mmoja akiwa ni wa gazeti la Habari Leo Bw. Anold Swai ambaye pia ni Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Hai, na mwingine ni mwadishi wa habari wa kujitegemea.
Swai na wenzake walikuwa wakitokea katika sherehe ya miaka 40 ya CCM ambayo kwa Mkoa wa Kilimanjaro zilifanyika wilayani Rombo.
Taarifa kutoka eneo la tukio zilieleza kuwa, Fuso ilifeli breki na kugonga gari hilo kwa nyuma kabla ya kuiparamia na kuigonga pikipiki na kusababisha vifo hivyo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi kutoka Mkoani humo imesema mbali na Swai, wengine waliofariki dunia ni pamoja na Anastazia Malamsha Mwenyekiti wa UWT (MoCu), Ally Mbaga (Mjumbe wa NEC) na Edwin Msele ambaye ni Katibu wa Hamasa Shirikisho la vyuo Vikuuu Moshi Mjini.
Wengine ni mwanamke mmoja ambaye jina lake halikupatina, Mwanamke mwingine aliyekuwa kwenye pikipiki iliyogonwa na Fuso naye hajafahamisha pamoja na mtu ambaye pia hajatambulika, wanaofanya jumla ya vifo kuwa saba, yaani watano waliokuwa kwenye gari hiyo na wawili waliokuwa kwenye pikipiki.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment