Image
Image

Watanzania tuipe msaada wa kila hali Serengeti Boys.

Vijana hao waliangua kilio baada ya Serengeti Boys kufungwa bao 1-0 na Congo katika mchezo wa marudiano uliofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Debat mjini Brazaville.
Matokeo hayo yalimaanisha kuwa matokeo ya jumla ya mechi mbili baina ya timu hizo yalikuwa mabao 3-3 baada ya Serengeti Boys kushinda magoli 3-2 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kwa kuwa Congo ilifunga mabao mawili jijini Dar es Salaam, matokeo hayo yaliwapa tiketi ya kuingia fainali za Afrika za vijana kwa sheria ya bao la ugenini.
Lakini Tanzania ikakata rufaa kupinga Congo kumtumia mchezaji aliyeonekana kuwa na umri mkubwa anayeitwa Langa-Lesse. Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) liliamua kuitaka Congo kumpeleka mchezaji huyo Cairo kwa ajili ya vipimo, lakini taifa hilo halikumpeleka kwa madai kuwa anatokeo eneo ambalo lina vita.
Ndipo CAF ikaamua kuipokonya ushindi huo baada ya kushindwa kumpeleka tena mchezaji huyo ilipopewa muda zaidi.
Kwa maana hiyo, Serengeti Boys ikapewa ushindi na hivyo kufuzu kwa mara ya kwanza kucheza fainali hizo zitakazofanyika Gabon baada ya Congo kupokonywa uenyeji kutokana na kosa hilo. Congo pia imefungiwa kushiriki mashindano yanayohusisha umri kwa miaka miwili.
Tunalipongeza Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa mkupigania haki hiyo hadi ikapatikana na hivyo kutoa nafasi kwa vijana wetu kwenda kupambana na kuonyesha vipaji vyao kwenye mashindano hayo muhimu.
Kinachotakiwa sasa ni kuipa Serengeti Boys maandalizi ya kutosha na msaada wa hali na mali ili kutuwakilisha kikamilifu fainali za Gabon.
Ni wazi kuwa ushindi wa timu nyingi unatokana na wachezaji kujiamini, kujengwa kisaikolojia na pia kujituma.
Pia ni muhimu kwa TFF kuandaa programu mahususi ya kuelekea fainali hizo, ikihusisha tathmini ya wachezaji hao kiumri na kuandaa akiba kubwa ya wachezaji kwa kujua kuwa chochote kinaweza kutokea kati ya leo na fainali hizo zitakapoanza.
Hii ni kwa sababu wachezaji wengi wenye umri chini ya miaka 17 hawapati nafasi kwenye vikosi vya kwanza vya timu zinazoshiriki Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza au Ligi Daraja la Pili, wakati hakuna mashindano ligi ya vijana ambayo makocha wanaweza kuyatumia kupata wachezaji zaidi wa kuboresha kikosi chao iwapo kutaokea upungufu.
Kwa kuwa fainali zinajumuisha wachezaji wachache kutoka nchi moja--wasiozidi 23-- ni wazi kuwa kufuzu kwa mashindano hayo kutaifungua macho TFF ione haja ya kuhakikisha klabu za Ligi Kuu zinakuwa na vikosi vya vijana kama masharti ya leseni za klabu yanavyotaka.
Bila ya kuwa na mashindano ya vijana, mafanikio hayo ya Serengeti Boys yatakuwa ya muda mfupi na hayatamaanisha maendeleo katika soka la Tanzania.
Tunapenda tena kuipongeza TFF na Serengeti Boys, makocha na wachezaji kwa kuwezesha bendera ya Tanzania kupeperushwa katika fainali za vijana za Afrika. TFF itumie mafanikio hayo kama chachu ya kuanzisha programu imara ya maendeleo ya vijana.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment