Image
Image

Rais Magufuli Amwapisha Jenerali Venance Mabeyo kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.

Rais John Magufuli leo amemuapisha Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi nchini , Jenerali Venance Mabeyo (Pichani) Ikulu jijini Dar es Salaam.
Jenerali Mabeyo aliteuliwa na Rais Magufuli Alhamisi iliyopita kushika wadhifa huo baada ya Jenerali Devis Mwamunyange kustaafu.
Jenerali Mabeyo alikuwa Luteni Jenerali kabla ya kupandishwa cheo kuwa Jenerali.
Kabla ya kuapishwa Jenerali huyo, Rais John Magufuli alimvalisha Luteni Jenerali Venance Mabeyo cheo kipya na kuwa Jenerali.
Pia, Rais Magufuli amemuapisha Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Luteni Jenerali James Mwakibolwa akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Mabeyo.
Aidha Rais Magufuli ameongeza kwa kusema kuwa anatambua kazi aliyoifanya aliyekuwa mkuu wa majeshi nchini Jenerali Davis Mwamunyange katika kipindi chote alichokuwepo mpaka muda wake kumalizika.
Amemtakia Mwamunyange kustaafu kwema kwani ataendelea kumkumbuka tu na kikubwa ni kumuombea huku akisema kuwa muda wa Mwamunyange licha yakuwa ulikuwa umeisha lakini hakutaka kwanza apewe mtu mwingine mpaka safari aliyokuwa ameenda arudi kwani angefanya maamuzi ingeonekana kama kamtumbua mkuu wa majeshi kumbe hapana.
Rais amekiri kufurahishwa na kazi nzuri ya Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange. 
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment