Mwandishi
wetu, Arusha
Ndoto ya kuwa na kijiji cha dijitali nchini Tanzania itaanza kutimia Januari
mwakani wakati vifaa vinavyotakiwa kukamilisha mradi huo vitakapowasili
kutoka kampuni ya Samsung Electronics.
Kwa mujibu wa watekelezaji wa mradi huo mkubwa unaotarajiwa kutumia dola za Marekani milioni 1, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) vifaa hivyo vinatarajiwa kuingia Bandari ya Dar es Salaam Januari tano mwakani.
Mkataba wa kuanzishwa kwa kijiji cha dijitali eneo la Ololosokwan tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro ulitiwa saini kati ya Unesco na Samsung electronics Novemba 6 mwaka huu.
Akizungumza na halmashauri ya kijiji cha Ololosokwan ,Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues amewataka wanakijiji kujiandaa kwa mabadiliko makubwa ya kijiji chao kinapoingia katika dunia ya dijitali.
Alisema mambo ambayo wanastahili kuyaweka sawa ili kufanikisha ndoto zao
kuhakikisha eneo ambalo mitambo na miundombinu ya mradi ipo ni lazima
lisajiliwe kisheria ili kusiwepo na tatizo katika siku za usoni.
Aidha kutokana na ukubwa wa mashine zinazohusika, hasa makontena ni vyema wanakijiji wakaangalia maeneo korofi katika barabara za kuelekea huko na kuzirekebisha, ili magari hayo makubwa yenye vifaa yapite kwa usalama.
Alisema mradi huo wa miaka mitatu unatarajia kuwawezesha wananchi wa eneo hilo kuwa na ujasirimali, matumizi ya teknolojia ya kisasa katika mawasiliano na utafutaji wa masoko, elimu na afya.
Kwa mujibu wa Bi. Rodrigues kijiji hicho pia kitakuwa na shule iliyoungwa na mtandao wa kompyuta duniani (intaneti), kliniki ya kisasa, tiba kwa kutumia teknolojia ya kompyuta na jenereta kubwa linalotumia nishati ya jua.
Aidha
kuwapo na mtandao wa kompyuta kutawezesha UNESCO kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuanzisha mtaala utakaowawezesha vijana wa kimasai ambao ni wafugaji kupata elimu wanayoihitaji.
Mwakilishi huyo wa UNESCO amesema kwamba amefurahishwa na namna watu walivyoitikia mradi huo ambao umelenga kubadili maisha ya wafugaji hao kwa kuwawezesha pia kuitumia vilivyo sekta ya utalii.
“Kupitia mradi huu wananchi wanaweza kujifunza kusoma, kupata maarifa na katika harakati hizo kujua lugha ya kiingereza ili kuwasaidia kuwa na
mawasiliano na watalii na watu wengine”, alisema Rodrigues.
Alisema ni nia ya Unesco kuhakikisha kwamba inasaidia kufuta ujinga miongoni mwa wafugaji hao bila kuathiri utamaduni wao wanapoingia katika maisha ya kisasa.
Kijiji cha digitali cha Ololosokwan kitakuwa cha nne
barani Afrika na yapo makubaliano ya msingi kwamba kijiji kingine
kitajengwa Zanzibar mwakani.

0 comments:
Post a Comment