KUNA
sababu nyingi za kuacha kukaa na badala yake mtu kufanya kazi akiwa
amesimama. Lakini kupunguza uzito pengine si moja kati ya hizo, kwa
mujibu wa utafiti mpya ambao umepima kwa usahihi kiasi cha kalori
ambacho watu hupunguza wakati wa shughuli za kila siku za ofisini.
Matokeo
ya utafiti huo mpya yanaonyesha kufanya mara nyingi kitendo cha aina
moja wakati mtu akiwa kazini huweza kutusaidia kuepuka kuongezeka uzito. Lakini kitendo hicho cha aina moja si kusimama. Wengi
wetu hukaa zaidi kuliko kusimama, na muda wetu mwingi wa kukaa hutumika
kazini, kwa sababu kazi nyingi za siku hizi ni za kukaa. Wengi wetu hutumia saa sita mpaka saba tukiwa kwenye meza zetu kila siku. Muda
huu mwingi, wa kutoshughulisha miili umehusishwa na ongezeko la hatari
ya kupata kisukari, ugonjwa wa moyo, vifo vya haraka na, lakini muhimu
pia, kuongezeka uzito. Katika
kupambana na hilo, wengi wetu, nikiwemo mimi, tumeanza kutafuta njia za
kupunguza muda wa kukaa. Tumepakua 'apps' kwenye smartphone zetu ambazo
hutukumbusha kusimama mara kadhaa ndani ya saa moja. Mabosi
wenye kuzingatia afya wameandaa mikutano ya kutembea, ambapo
wafanyakazi hujadiliana masuala ya kazi huku wakitembea kwenye kumbi. Na
meza za kusimama zimekuwa maarufu. Utafiti
uliofanyika hivi karibuni umeonyeha kuwa maamuzi ambayo hutuinua kwenye
viti vyetu yanaweza kutusaidia kudhibiti kiasi cha sukari kwenye damu
na kupunguza hatari ya kupata kisukari na magonjwa sugu. Lakini cha
msingi zaidi hali halisi ni kinyume kwani wengi wetu tunainuka kwenye
viti kwa matarajio kuwa kukaa muda mfupi kutasaidia kutonenepeana. Katika
hali ya kushangaza tafiti chache, hata hivyo, zimefuatilia kwa karibu
kiasi cha ziada cha kalori ambacho hupungua kama tutasimama ama kutembea
tembea katika ofisi zetu. Hivyo
katika utafiti mpya, ambao ulichapishwa katika jarida la mwezi huu la
'Journal of Physical Activity and Health' (Jarida la Mwili
Kujishughulisha na Afya), watafiti katika Chuo Kikuu cha Pittsburgh,
hapa Marekani walikusanya watu 74 wenye afya zao waliojitolea. Wengi
wlaikuwa katika umri wa miaka ya katikati mwa 20, wa uzito wa kawaida,
na wenye uzefu wa maisha ya ofisini. Watu
hawa, bila ya utaratibu maalumu, walipangwa katika makundi manne. Kundi
moja lilitakiwa kukaa na kuchapa katika kompyuta kwa dakika 15 na kisha
kusimama kwa dakika 15, kisha kuzunguka zunguka ofisini humo. Kundi
lingine lilikaa kwa dakika 15, lakini liliangalia televisheni bila ya
kupiga chapa kwenye kompyuta. Baadaye, wakahamia kwenye mashine ya
mazoezi haraka na kutembea kwa dakika 15 kwa mwendo wa pole.
Kundi la tatu lilisimama kwa dakika 15 kisha likakaa chini kwa dakika 15. Na kundi la mwisho lilitembea kwenye mashine ya mazoezi kwa dakika 15 kisha kukaa. Wakati
wote, watu hao walivaa vifunika uso ambavyo vilirekodi kiasi cha nguvu
wanchotumia, kitu kinachomaanisha kiasi gani cha kalori wanapoteza. Kama
ilivyotarajiwa, kukaa hakukuchukua kiasi kikubwa. Watu hao wlaipoteza
kalori 20 katika dakika 15 za kukaa, iwe walikuwa wakipiga chapa kwenye
kompyuta au kutazama televisheni. Kama
ilivyotarajiwa zaidi, kusimama hakukuwa na tofauti sana. Wakiwa
wamesimama kwa dakika 15, watu hao walipoteza kalori mbili zaidi
kulinganisha na wakati walipokuwa wamekaa. Haikujalisha kama walikaa
kisha wakasimama ama walikaa kisha wakasimama. Kiasi cha kalori
walichotumia kilikuwa kama kilicholingana na hakikuwa kikubwa. Kwa
ujumla, ni kwamba, watafiti waliamua, mtu aliyesiama akiwa kazini
badala ya kukaa atapoteza kalori nane mpaka tisa zaidi kwa saa. (Kwa ajili ya kupata picha halisi, kikombe kimoja cha kahawa ya maziwa na sukari kina kalori 50.)
Lakini kutembea ilikuwa habari nyingine. Wakati
watu hao walipotembea kwa dakika 15, hata taratibu tu, walipoteza mara
tatu ya kalori kulinganisha na wakati walipokuwa wamekaa au kusimama. Kama
wangetembea kwa saa moja, watafiti walipiga hesabu, wangepoteza kalori
130 zaidi kama wangekuwa wamekaa kwenye viti vyao ama kusimama kwenye
madawati yao, matumizi ya ziada ya kalori ambayo yangetosha, wameandika,
kusaidia watu kuepuka ongezeko hatari la uzito wa mwili la kila mwaka. Hitimisho
la utafiti ni kwamba kama lengo lako kazini ni kudhibiti uzito wako,
basi “kusimama kunaweza kusitoshe,” anasema Seth Creasy, mhitimu wa Chuo
Kikuu cha Pittsburgh na muandishi mkuu wa utafiti huo mpya. Utatakiwa
pengine kujumuisha pia kutembea katika matendo yako ya kazini, anasema.
Pengine “weka printa kwenye chumba kingine cha mbali, au simama uende
kwenye friji la maji kila baada ya saa hivi” badala ya kuweka chupa ya
maji kwenye meza yako. “Dakika
chache za kutembea zinaweza kujumlishwa na kuleta tofauti kubwa” katika
matumizi ya kalori, alisema, wakati kusimama hakuchomi kalori
'kihivyo'. Ni
kweli, kusimama kuna faida nyingine kiafya mbali na kudhibiti uzito wa
mwili, Creasy alisema, ikiwemo udhibiti bora wa sukari ya damu na
upungufu wa maumivu ya mgongo na kiuno yanayohusishwa na kukaa kutwa
nzima kwenye kiti. Hivyo
usivunje wala kutupa tabia ya kusimama kwa kusimama. Lakini usiitegemee
kukusaidia kuondoa sukari uliyobugia kwa njia ya chakula kwenye mlo wa
mchana. New York Times
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment