Rais John Pombe Magufuli amempongeza mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Magu kwa kitendo cha kuwasimamisha kazi askari wake waliotuhumiwa kujihusha na biashara za dawa za kulevya ili kupisha uchunguzi na hivyo kulipa heshima jeshi hilo.
Amesema hayo hivi leo mara baada ya kumuapisha Mkuu wa Majeshi nchini Jenerali Venance Mabeyo Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa suala la dawa za kulevya haliangalii umaarufu wala jina la mtu hivyo amevitaka vyombo vinavyohusika kuishughulikia suala hilo kwa kina zaidi ili kuweza kutokomeza kabisa biashara ya Dawa za kulevya nchini.
"Najua IGP Mangu watu walikupigia simu wanakupa ushauri kuhusu Dawa za Kulevya, ungewasikiliza leo usingekuwa IGP, Vita ya dawa za kulevya haina cha umaarufu, haijalishi ni mtoto wa nani anahusika, hata kama ni mke wangu mkamateni"Amesema Magufuli.
Rais Magufuli amekiri kuwa suala la kukabiliana na biashara hiyo ya dawa za kulevya na matumizi yake nikubwa licha ya kwamba ni vita ngumu mno lakini kwa kumtanguliza mungu itawezekana, kuanzia Tanzania bara mpaka Visiwani kwakuwa sio suala la mtu mmoja nilawatu wote ili kuweza kutokomeza kabisa mizizi ya Biashara ya Dawa za kulevya.
Hata hivyo Rais Magufuli amemuomba Jaji Mkuu asizicheleweshe kesi za dawa za kulevya, ametaka kesi zinazohusu dawa za kulevya ziharakishwe kwa watu wanaokamatwa na zisicheleweshwe ikiwa inajulikana wahusika na ushahidi ukiwa upo wazi, kwakuwa suala hilo haliangalii mkubwa fulani, ili sheria ichukue mkondo wake.
"kwani kuna mtuhumiwa mkubwa wa Dawa za Kulevya anashikiliwa Lindi bila ya kufikishwa Mahakamani"Amesema Magufuli.
Aidha Rais ameongeza kwa kusema kuwa kuhusu suala hilo la kupambana na wauza dawa za kulevya hakuna wa kuachwa hata kama angekuwa mkewe Mama Janet Magufuli,huku akisema suala hili watu wasije kudhani nilamakonda pekee.
Rais Magufuli amelipigilia msumari suala la wafanya biashara wa dawa za kulevya ikiwa nisiku chache baada ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuwataja askari ambao wanatuhumiwa kwenye sakata hilo hali ambayo ilimladhimu mkuu wa Polisi IGP Ernest Mangu kuwasimamisha kazi askari 12 ili kupisha uchunguzi.
Mbali na askari pia Makonda aliwataja wasanii ambao nao wanahusika na biashara hiyo ya dawa huku akiwataka wajisalimishe kituo cha polisi ambapo baadhi yao walijisalimisha ambapo wasanii maarufu wa muziki na filamu akiwemo Wema Sepetu, Chid Benz, Vanessa Mde, Nyandu tozi,Dogo Hamidu,T.I.D,Mr.Blue n.k.
Mbali na askari pia Makonda aliwataja wasanii ambao nao wanahusika na biashara hiyo ya dawa huku akiwataka wajisalimishe kituo cha polisi ambapo baadhi yao walijisalimisha ambapo wasanii maarufu wa muziki na filamu akiwemo Wema Sepetu, Chid Benz, Vanessa Mde, Nyandu tozi,Dogo Hamidu,T.I.D,Mr.Blue n.k.
0 comments:
Post a Comment