Image
Image

HII NDIO HOTUBA ILIYOCHACHAFYA BUNGE NA KUAHIRISHWA.


Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana liliahirishwa baada ya Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje (CHADEMA) kukataa kuomba radhi,  Marekebisho ya hotuba ya upinzani kuhusu CUF na ushoga.

 Haya hapa Mabadiliko katika ukurasa wa 8 aya ya pili inayoanza na maneno ‘Mheshimiwa Spika, Kwa upande wa chama cha CUF.... na kuishia na maneno… Israel Liberal ‘ sasa isomeke:

“Mheshimiwa Spika, kwa upande wa chama cha CUF, kutokana na itikadi zake za mrengo wa Kiliberali chama hicho ni mwanachama wa Umoja wa Vyama vya Kiliberali Duniani (Liberal International). 

Kwa mujibu wa tovuti ya umoja huo CUF imejiunga na Oxford Congress ya Liberal International Mwaka 1997.

Mwaka huo huo Liberal International ilitoa msimamo wa pamoja wa umoja huo uliotwa Liberal Manifesto (Ilani ya Kiliberali) ya 1997 iliyopitishwa katika mkutano mkuu wake wa 48 uliofanyika tarehe 27 mpaka 30 Novemba 1997 katika ukumbi wa Mji wa Oxford nchini Uingereza. 

Katika ilani hiyo ya waliberali, umoja wa vyama hivyo ulikubaliana msimamo wa pamoja, nanukuu: “the extension of the rules of equality to sexual minorities and the recognition that homosexuality and lesbianism are legitimate expressions of personal proclivities”. 

Kwa Tafsiri rahisi waliberali hao walipitisha ajenda ya waliberali katika karne ya 21 (The Liberal Agenda in the 21st Century) ya kuutambua ushoga na usagaji kama matendo halali. 

Hii ni kwa mujibu wa tangazo la Umoja huo kwenye mtandao wao wa waliberali ulimwenguni, likiungwa mkono na Waziri wa Haki na Usawa wa Uingereza, Lynn Featherstone kutoka chama cha Liberal Democrats wakati chama hicho (Liberalism) kilipokuwa kinapitisha azimio la kuruhusu ndoa za jinsia moja kama haki ya mtu mmoja mmoja.

Kupitia umoja hao CUF inashirikiana na vyama vingine kama vile LPC ya Canada, Det Radikale Venstre cha Norway, FDP cha Ujerumani, Israel Liberal………” 

Ezekiah Dibogo Wenje 
Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni 
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa 
30 Mei 2013

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment