Image
Image

WATU WATATU WAMEUAWA KWA KUKATWA KATWA MAPANGA NA KUCHOMWA MOTO HUKO BUNDA MKOANI MARA.


Kamanda wa polisi Mkoani Mara kamishina msaidizi Mwandamizi Absalom Mwakyoma amesema kuwa tukio hilo limetokea wilayani Bunda ambapo limehusishwa na Imani za Kishirikiana.

Kamanda Mwakyoma amesema kuwa tukio  hilo linafuatia tukio lilotokea April 15 Mwaka huu ambapo  Daudi Samson au Phares Wegero mwendesha Pikipiki aligongwa na gari na kufariki dunia ambapo baada ya hapo ndugu zake walienda kwa Mganga wa Jadi na kuambiwa kuwa Marehemu hao wamehusika katika kifo cha kijana huyo.

ABSALOM MWAKYOMA - KAMANDA WA POLISI MARA
Kamanda Mwakyoma amesema mpaka sasa jeshi Hilo linawashikiria watu kadhaa kutokana na Mauaji hayo huku akiwataka wananchi wenye taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo kutoa taarifa hizo kwa jeshi la Polisi
 
Waliouawa katika tukio hilo ni pamoja na Tibezuka Biseko au bibi Rai mwenye umri wa miala 75), Chausiku Rubisha 73 na Mugara Manyama 68 wakazi wa kijiji cha Kasahunga wilaya ya Bunda Mkoani Mara.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment