Image
Image

EXCLUSIVE: MICHELLE OBAMA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MAMA SALMA, ASEMA WANAWAKE NA WATOTO SASA KUNUFAIKA NA MAENDELEO


Na. Esther Zelamula Dar Es Salaam
Washiriki Mbali mbali wa kiserikali wakiwa wapo kwenye ofisi za wama ambapo  Michelle obama wakati akifanya mazungumzo na mama kikwete leo wakiwa wanafuatila.

Mke wa rais wa Marekani Michelle Obama aliyeko nchini akiambatana na mumewe kwa ziara ya siku mbili leo amekutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake mke wa rais wa Tanzania Mama Salma Kikwete jijini Dar es salaam.
Mama Salma Kikwete (Kulia) Akipiga picha ya Pamoja na Mke wa Rais Obama Michelle obama kwenye ofisi za Wama leo jijini Dar es Salaam.. 


Baadhi ya washiriki wakifurahi mara baada ya Mke wa Rais Obama Michelle obama  kuwasili nchini Tanzania akiwa na mumewe kwa dhumuni la ziara ya siku mbili, ambapo alipata fursa yakufika katika ofisi za maendeleo ya wanawake Wama huku Mwenyeji wake akiwa Mama salma Kikwete.
Akiwa kwenye ofisi za taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) ambayo Mwenyekiti wake ni Mama Salma Kikwete, Mama Obama alipata fursa ya kupiga picha na mwenyeji wake Mama Kikwete  na baadaye kuzungumza masuala mbalimbali yaliyolenga kunufaisha jitihada za WAMA katika kuleta maendeleo kwa wanawake na watoto wa Tanzania.
Mama Salma Kikwete (Kulia) Akisalimiana na Michelle obama kwenye ofisi za Wama leo. 
Mara baada ya kuzungumza na Mama Kikwete, Mama Obama pia alipata fursa ya kutembelea Makumbusho ya taifa .
Mama Salma Kikwete (Kulia) Akiteta jambo na  Michelle obama kwenye ofisi za Wama Picha zote na (Semvua Msangi).
Hafla fupi ya kumkaribisha Mama Obama kwenye viwanja vya WAMA, imehudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa UN Dk. Asha Rose Migiro, Mke wa rais Mstaafu Mama Anna Mkapa, Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Sophia Simba na mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda.

Ujio wa Rais Barack Obama wa Marekani na familia yake hapa nchini, ni kielelezo tosha cha ushirikiano baina ya Tanzania na Marekani na ni fursa kwa wananchi na serikali yaTanzania katika jitihada za kuimarisha na kukuza uchumi wa Tanzania.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment