Image
Image

M23 YAZITISHIA FAMILIA ZA WAHANGA HUKO DRC KONGO.


M23


Mwanaharakati mmoja wa kutetea haki za binadamu amesema kuwa, waasi wa M23 wanazitishia familia za wahanga ambao walioko kwenye mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda wasitoe taarifa zozote zilizokuwa dhidi yao kwa shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch.

 Mwanaharakati huyo ambayo hakuwa tayari kujitambulisha wasifa wake amesema kuwa, waasi wa M23 wamekuwa wakizituhumu familia za wahanga kwa kutoa taarifa zao kwa shirika hilo la kutetea haki za binadamu.

 Shirika la Human Rights Watch hivi karibuni lilitoa taarifa na kueleza kuwa, waasi wa M23 walioko mashariki mwa Kongo waliwahukumu adhabu ya kifo watu 44 bila ya kuwafungulia mashtaka katika jimbo la Kivu Kaskazini mashariki mwa Kongo, kwa makosa ya kuwabaka wanawake na wasichana 61 na kuwafanyisha kazi kwa nguvu watoto wadogo.

Wakati huohuo, waasi wa M23 wanawashikilia vijana wasiopungua 50 kwa tuhuma za kushiriki kwenye maandamano yaliyopelekea kuchomwa moto maduka ya watu wanaozungumza lugha ya Kinyarwanda huko mashariki mwa Kongo. Hayo yameelezwa na Luteni Kanali Vianney Kazarama Msemaji wa kundi la waasi wa M23.   
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment