Image
Image

PANDU: BARAZA LA WAWAKILISHI LIWE NA TAHADHARI WAKATI WA KUFANYA MAAMUZI.


Pandu ameir kificho - Spika wa Baraza la wawakilishi Zanzibar. 
Ali Issa- Zanzibar.

Spika wa baraza la wakilishi Zanzibar Pandu ameir kificho amesema Baraza la wakilishi liwe na Tahadhari sana kufanya maamuzi ambayo utekelezaji wake umo katika mikono ya Serikali ili kuiepusha Serikali kuja kuingia katika kitahanani kwa lile amblo kulitimizia Taifa mahitaji yake muhimu.

Hayo ameyasema  leo huko Baraza la wakilishi  wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi kwa mwakilishi wa Kwamtipura CCM  Hamza Hassan Juma wakati alipokuwa amezuia kifungu kuipitisha Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kusema uagiziaji wa kuku kutoka Nnje uzuuliwe kwani una uwasokosesha mapato wafugaji wa ndani na kuliua soko lao.

Amesema si vyema kutoa maamuzi ya moja kwa moja kulilazimisha hilo kuzuia kuku kutoka nje wasiletwe nchini bila ya kuwa na utafiti wakutosha utao bainisha wazi kuwa hawahitajiki kuku wa nje.

 “sivizuri kuzuia fungu hili na kukusema kuku wasiagiziwe kutoka nje bali tuwachie Serikali wakachunguze ukweli wa hilo na baadae watuleteeripoti,”alisema Spika.

Aidha ali sema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina wapenda sana wananchi wake kuona kua wanafanikiwa katika uzalishaji kwani ndio lengo la Serikali yao kujikwamua na umasikini na kujipatia kipato wawe makini kuliko kuchukuwa maamuzi ya haraka.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment