Image
Image

SERIKALI KUPOKEA MAPENDEKEZO YA KODI KWENYE LAINI ZA SIMU



Serikali imesema inaendelea kupokea mapendekezo kutoka kwa wadau mbalimbali ili kuona jinsi ya kupunguza makali ya Kodi ya shilingi elfu moja kwenye 'sim card' hususan kwa wananchi wa kipato cha chini.


Waziri wa Fedha, Dk.William Mgimwa amesema nia ya serikali ni njema na kwamba kodi hiyo inalenga kuboresha huduma ya maji umeme na barabara vijijini.
Dk.William Mgimwa - Waziri wa fedha Tanzania.
Dk.Mgimwa ambaye alifuatana na Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia, Prof.Makame Mbarawa wamefanya Mkutano wa Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam ambapo wamezungumzia mapendekezo yaliyowasilishwa serikalini na Mtoa Huduma za Mawasiliano.

Prof.Makame Mbarawa - Waziri wa Mawasiliano sayansi na Teknolojia Tanzania.
Hatua ya Serikali  kuamua kukata kodi ya shilingi elfu moja kwenye 'Sim Card' imeibua manung'uniko makubwa kutoka kwa wadau wa mawasiliano hapa nchini ambapo wamedai kodi hiyo ni mzigo mzito kwa wananchi wa kawaida.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment