Image
Image

JESHI LA POLISI KITENGO CHA USALAMA BARA BARANI, TUSIWAFUMBIE MACHO BODA BODA WAZEMBE WANATUMALIZA.

Kama kweli tunataka kuliokota taifa na janga la ajali za pikipiki ni lazima waendesha pikipiki waheshimu utawala wa sheria. Dereva kama hana mafunzo ya udereva au leseni, asiruhusiwe kuendesha chombo cha moto. 


Huu ndio usafiri wetu wa haraka dar lakini kwa mikoa mingine haya ndio magari, piki piki hizi nimevutiwa nazo leo hii katika kituo uchwara Tabata kinyerezi zikiwa zimepaki kwa kusubiria abiria.




Huu ndio usafiri wetu wa haraka dar lakini kwa mikoa mingine haya ndio magari, piki piki hizi nimevutiwa nazo leo hii katika kituo uchwara Tabata kinyerezi zikiwa zimepaki kwa kusubiria abiria.



TANGU Serikali ya Tanzania iridhie pikipiki maarufu kama bodaboda kubeba abiria, tumeshuhudia ndugu na marafiki zetu wakipoteza maisha na hakuna ubishi sasa ni janga la kitaifa.


Inavyoonekana, wakati Serikali ikiruhusu pikipiki kubeba abiria ilikuwa haijajiandaa kikamilifu na badala yake ilijikita kuangalia mapato ya kodi yatakayotokana na biashara ya kubeba abiria na kikubwa zaidi kutengeneza ajira kwa vijana.



Naamini Serikali haikujiandaa kwa sababu leo hii si ajabu kijana kujifunza pikipiki kwa dakika 30 na kuingia barabarani kubeba abiria. 

Serikali iko kimya!.

Takwimu zinatuonyesha tangu 2009 serikali ilipokubali pikipiki kubeba abiria mpaka mwaka jana, pikipiki 330,882 zimesajiliwa nchini sawa na asilimia 60 ya usafiri huo.


Ongezeko hilo la pikipiki limekuja na janga lingine kwa Watanzania. 

Vifo na majeruhi wamekuwa wakiongezeka siku hadi siku na kuwasababishia baadhi ya vijana na abiria ulemavu wa kudumu.

Sababu kubwa ya vijana na abiria wa pikipiki kupata ulemavu wa kudumu ni uzembe wa madereva uchwara kufanya kazi hiyo.



Tunaambiwa mwaka 2011 pekee, kulikuwapo ajali 5,384 za pikipiki zilizosababisha vifo vya watu 945 na majeruhi 5,506, wakati mwaka 2010 kuliwapo ajali 4,463 zilizosababisha vifo vya watu 683 na majeruhi 4,471.

Takwimu za hivi karibuni kabisa–Januari mpaka Septemba 2012 kulikuwapo ajali za pikipiki 4,142 zilizosababisha vifo 720 na kuwaacha Watanzania wenzetu 4,057 wakiwa walemavu.



Nimeanza kwa kuweka takwimu hizo ili ninaposema suala la Bodaboda sasa ni janga la kitaifa, Watanzania na mamlaka zinazohusika ikiwamo rafiki zangu trafiki waone ukubwa wa tatizo.


Hakuna ubishi kwamba mamlaka zenye dhamana za kusimamia usafiri huo zimelala na kusababisha kuwapo kwa walemavu na watu wengi kupoteza maisha.



Si ajabu kukuta askari wa usalama barabarani wakiwa kazini, lakini vijana wakiendesha pikipiki bila leseni, na kutovaa kofia ngumu.



Sote tunafahamu, katikati ya mji tena kwenye msongamano mkubwa tumekuwa tukishuhudia wakiendesha kwa mwendo mkubwa tena mbele ya askari wa usalama barabarani?.


Tatizo ninalolioa hapa ni udereva kuchukuliwa kama sio taaluma, Ndio maana leo muuza urembo anaweza kununua pikipiki, hana leseni, wala hajawahi kuendesha pikipiki na akaanza kuendesha.


Huu sasa ni wakati wa kujifunza kwa jeshi la polisi na mwisho wa siku kuonekana kana kwamba ni wadhaifu hasa kikosi cha usalama barabarani kumbe ni watu wachache wanalipotezea sifa jeshi hilo



Sheria ziko wazi kwamba mtu hawezi kuendesha chombo cha moto bila kuwa na leseni tena aliyoipata kihalali, lakini wapo bodaboda wanakamatwa leo anahonga, kesho yuko tena barabarani.





Kama kweli polisi wetu wa usalama barabarani wangekuwa na ratiba za kazi kila siku kwamba leo tushughulike na bodaboda wasio na leseni, hakika tungepunguza ajali za pikipiki.

Si ajabu leo ukamuona mwendesha bodaboda akilipita (overtake) gari kupitia upande wa kushoto, anaonyesha taa akimaanisha anakata kulia, lakini anakata kushoto. 




Dereva kama hana mafunzo ya udereva au leseni, asiruhusiwe kuendesha chombo cha moto.




Tusihalalishe uvunjifu wa sheria kwani tutawapoteza vijana wengi kwa wanajisikia fahari kubwa kuendesha pikipiki kwa mwendo kasi bila kujali uhai wao.


Tuwasaidie vijana kwa kuwa wengi wao hajui wanalolifanya, polisi wa usalama barabarani wawakamate kuwaadhibu kwa mujibu wa sheria kwani kufanya hivyo ni kwa faida yao na watu wengine wanaotumia usafiri huo.






Kwa mtazamo wangu polisi wa usalama wa barabarani wanatakiwa kufanya operesheni maalumu ya kukamata pikipiki zote abazo zina makosa ya usalama barabarani.

Pili, waendesha bodaboda ambao watakutwa hawana leseni, hawataruhusiwa kuendesha mpaka waende shule na baada ya kufuzu waonyeshe cheti na leseni halali ya udereva.





Naamini kama tukiweka utaratibu huo hakika hakuna atayakeingia barabarani bila kuwa amepata mafunzo ya udereva na kujua alama za barabarani pamoja na sheria nyingine.






Haiwezekani leo ni mwaka wa tatu tangu Serikali iruhusu biashara ya Bodaboda bado wapo wanaoibuka na kuendesha pikipiki bila leseni wala kujua sheria za barabarani.





Trafiki wanatakiwa kuchukua hatua kali ya kuwadhibiti waendesha pikipiki ambao hawavai kofia ngumu, walevi, na waendesha pikipiki kwa kasi. 




Ni fedheha kwa jeshi la polisi kuwaachia waendesha pikipiki kuvunja sheria za usalama barabarani.
, Jambo lingine la kushangaza ni tabia ya waendesha pikipiki kusababisha ajali na kuwa wa kwanza kupigiana simu na kuharibu gari na wakati mwingine kuwajerihi gari ambalo limegongwa na dereva wa bodaboda.



Ni jambo la kushangaza! Kwanini, polisi wa usalama barabarani wametoa uhuru mkubwa kwa waendesha pikipiki? Wanachukua sheria mkononi na hakuna anayewauliza. 


Nadhubutu kusema pengine wanakula rushwa ya Sh2,000 hadi 10,000 kutoka kwa baadhi madereva wa boda boda.



Kutokana na hali hiyo kama polisi wasipojipanga upya kwa ajili ya kuwadhibiti waendesha bodaboda, usafiri huo utaendela kuwaua watu wengi.




Trafiki wetu watambue kwamba hakuna mahali mtu anaweza kununua uhai. 


Pia madereva bodaboda na abiria wajue hakuna duka la kununua uhai. 


Kila mmoja awajibike kwa mujibu wa sheria kulinda uhai wa mwenzie.






Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment