Image
Image

MWENDWA AFUKUZWA KAZI NA BOSI WAKE KWA KULIPALILIA PENZI LA MJANBE.



Mwanaume wa nchini Kenya ambaye aliridhia kusaini mkataba wa kuchangia mwanamke mmoja na mwanaume mwenzake amefukuzwa kazi na bosi wake.

Mwanaume huyo Sylvester Mwendwa, ambaye mwishoni mwa wiki alitangaza hadharani penzi lake hilo la mkataba na mwanamke mjane, amesema bosi wake amemfukuza kazi ya bucha aliyokuwa akiifanya baada ya kusikia habari hiyo.

Mwendwa ambaye alikiri kuwa na mapenzi ya dhati kwa mwanamke huyo na yuko radhi kufanya lolote ili aendelee kuwanae hata ikibidi kuchangia na mwanaume mwingine, amedai amekuwa akipokea ujumbe wa kutishiwa maisha yake.

Baada ya uhusiano wake na mwanamke huyo Joyce Wambui pamoja na mwanaume mwingine kujulikana kwa umma Mwendwa sasa amelazimika kukimbilia mafichoni akihofia usalama wa maisha yake.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment