Image
Image

IDADI KUBWA YA MATEKA WALIOSHIKILIWA NA WANAMGAMBO WA AL SHABAB WAOKOLEWA NA JESHI LA KENYA LIMEDHIBITI JENGO LA WESTGATE.




Waziri wa mambo ya ndani wa Kenya Joseph Ole Lenku amesema Idadi kubwa ya mateka wameokolewa na Jeshi la Kenya baada ya kudhibiti sehemu kubwa ya jengo la kibiashara Westgate katika operesheni ya kuhakikisha wanawakomboa mateka waliokuwa wakishikiliwa na wanamgambo wa kundi la Alshabab ambao walivamia na kuteka eneo hilo jumamosi mchana.

Ole Lenku ameongeza kuwa mpaka sasa Idadi rasmi ya watu waliopoteza maisha imefikia 62 wakati majeruhi wakifikia 175 wakati  wapiganaji wawili wa Alshabab wamethibitika kuuawa na wengine baadhi kujeruhiwa.

Misaada ya aina mbalimbali imeendelea kutolewa ikiwemo zoezi la uchangiaji damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya majeruhi ambao wengine wamefanyiwa upasuaji.

Tukio la mashambulizi yaliyofanywa na wanamgambo wa Al-Shabab kwenye maduka ya westgate nchini kenya limezusha hofu miongoni mwa mataifa ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi za Maziwa makuu.

Serikali za Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi zimelaani shambulio hili na kutoa pole kwa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na wananchi wa taifa hilo ambao wamepoteza ndugu zao.

Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa kenya kwasasa inakabiliwa na changamoto kubwa ya kiusalama hali ambayo ni lazima nchi jirani ziimarishe usalama kwenye mipaka yao.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment